Heche Amshukuru Spika Kwa Kumlinda Asikamatwe



Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amekiri bila busara za Spika wa Bunge kutumika leo angekuwa amekamatwa leo na polisi wamedaiwa kutoka Morogoro waliokuwa eneo la Bunge kwa nia ya kumkamata.

Mh. Heche amweka hilo wazi jioni hii huku akikosoa matumizi mabaya ya rasilimali iliyotumiwa.

"Nimepokea barua ya polisi asubuhi leo wakinitaka kuripoti Morogoro eti kwa kosa la kumsindikiza na kufanya mkutano jimboni kwa Mh Lijualikali alipotoka gerezani mwezi wa 4" Amesema Heche na kuongeza;

"Kabla hata ya kuitikia wanataka kunikamata bila busara za spika wangenikata. Matumizi mabovu ya rasilimali"

Kabla ya taarifa hii kutoka Mapema leo Heche alikiri kupokea wito unaomtaka kwenda kuhojiwa Morogoro.

"Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.

1 Comments

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post