Msemaji wa Klabu ya Soka ya Simba Haji Manara, amesema anampango wa kugombea urais na anaamini atafanikiwa.
Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Haji Manara amesema kazi zake anazofanya sasa zimemfanya aache hesima kubwa, kitu ambacho kinampa ujasiri wa kufikia uamuzi huo.
“Unajua mi nakwenda kuwa rais wa nchi siku moja, mimi nakwambia Mungu akinipa uhai na majaliwa, nakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, amesema Haji Manara.
Msikilize hapa chini na akitaja watu gani hatawaweka kwenye baraza lake la mawaziri.
Tags
kitaifa