Zitto Kabwe Achoshwa na Tambo za IGP na Amiri Jeshi Mkuu Mauaji ya Kibiti..Adai ni Maneno Matupu tuu



Watu 2 wanahofiwa kuuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti kuamkia leo, Kamanda Lyanga amesema wanafuatilia tukio hilo ili kujua ukweli wake.

Kufuatia taarifa hizo za kuuawa kwa watu wawili Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe amefunguka juu ya mauaji yanayoendelea kutokea mkoa wa Pwani eneo la Kibiti kwa kuitaka serikali itazame jambo hilo kwa mtazamo mpana kwa kuwa wananchi wana haki ya kujua nini kinachoendelea juu ya mauaji hayo.

Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake Facebook huku akidai kuwa Usiku wa kuamkia leo yameweza kutokea mauaji mengine ambayo yamepelekea kuuwawa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kata ya Mchukwi na Mwenyekiti wake kwa kupigwa risasi na baadaye kuchomwa moto nyumba zao.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post