Wema sepetu atoa povu kwa wanaojadili umbo lake

Malikia wa filamu Bongo Wema Sepetu 'Tz Sweethert'  amejinadi kwamba huwa hamalizi kujitazama umbo lake alilopewa na Mungu huku akiwataka wale ambao hawajajaaliwa na wamshukuru pia Mungu


Kauli hiyo ameitoa kwenye mtandao wake wa wa kijamii baada ya hivi karibuni kutupia picha zilizochora shepu yake kucua utata huku wengine wakimnanga kwamba siyo ya aili na imefika magotini.

"Shepu ya mwendokasi.. Ndiyo niliyojaliwa nayo... Kama imeanzia kiunoni kwenda magotini ndiyo niliyojaliwa nayo, Ndivyo nilivyoumbwa jamani... Sio mimi bali ni Maulana ndo alionibariki nayo... Hata ingekuwa kuanzia kichwa hadi vidole vya miguuni ni sawa pia... Ndiyo niliojaliwa nayo.... Sometimes najiangalia kwenye kioo sijimalizi... Ndo majaliwa yangu. Ndo yangu basi..Imenizidia....Allah Subhanah wataallah ndo amenipa... Aaaah....!" Wema alisema.

Aidha Wema ameongeza kwamba Sio shepu ya kawaida... Niacheni na Shepu yangu jamani.. Ndo nimeshaimiliki mie... Siwezi kuitoa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post