Doreen wa Lucky Vincent bado yupo wodini na anaendelea vizuri

UPDATE:-
KUTOKA Mercy Hospital, Sioux City IA
Jumanne, Mei 30
Saa 3:40 Asubuhi (Saa za Afrika Mashariki)

MTOTO Doreen: Malkia wa Roho za Watanzania:-
AKIWA ameendelea kuwepo katika WODI ya WATOTO Mercy Hospitalini, MTOTO Doreen ameelezewa KUENDELEA kuimarika na MWILI wake kuitikia MATIBABU anayoendelea NAYO. MTOTO Doreen  alifanyiwa UPASUAJI kwenye "hip" (Chini ya Kiuno), kwenye bega, kwenye kidevu, na mwisho kwenye UTI WA MGONGO. Katika UMRI wake, AMEJARIBIWA na KUUMIZWA kusiko elezeka.
SASA, akiwa PICHANI na Mama yake saa 4 :00 asubuhi (Saa za CST-Sioux City IA), MTOTO Doreen amekuwa JIBU la MAOMBI ya wengi. Hakika MUNGU ni mwema!  Watoto wetu wako salama mikononi mwake. USHUHUDA wa Doreen utukumbushe SOTE kuwa MUNGU akitaka KUKUBARIKI, hakuna awezaye KUZUIA. Tuendelee KUMWOMBEA***
(Picha kwa hisani ya DMS, Sioux City IA, Leo)

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post