Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka sababu za kuacha kuendelea kuisapoti CHADEMA ni viongozi wa chama hicho kushindwa kuutambua mchango wake alioutoa wakati wa uchaguzi mkuu hali iliyomfanya ajihihisi mpweke na kama ametelekezwa .
Ikiwa ni mara ya kwanza Wolper kufunguka ishu hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kwenye ukurasa wa facebook EATV, amesema hajawai kuwa msaliti kwani hakuwa mwanachama wa chama hicho lakini alisikitishwa na uongozi wa chama kushindwa hata kumshukuru kwa kazi aliyoifanya wakati wa uchaguzi mkuu kwa kujitoa pasipo kulipwa hata shilingi elfu 10 za kitanzania.
Pamoja na kuwa alifanya kampeni za kumsapoti Mgombea uraisi kupitia mwamvuli wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa, Wolper amedai kuwa hakuwa anasapoti chama kizima bali mgombea kwa kuwa yeye ni shabiki wa kiongozi huyo na familia yake kwa ujumla ndiyo maana hakukubali kulipwa katika kampeni hizo.
"Mimi nilifanya siasa kwa sababu namkubali Lowassa, na mimi ni shabiki wake na familia yake kwa ujumla. Nilianza kumsapoti Lowassa tangu yupo CCM. Mimi ni mfanyabiashara na muigizaji, sijawahi kuwa mwanasiasa ndio maana nilikuwa namsapoti mtu mmoja mmoja na siyo chama. Hata hivyo mimi siyo Yuda kwa CHADEMA kwa sababu sijawahi kuwa mwanachama wao na sina chama chochote lakini wao baada ya uchaguzi walinitelekeza kiasi cha kunifanya nijisikie mpweke. Hata kama hawakushinda uchaguzi walipaswa hata viongozi wawili wanishukuru tu kwa maneno ili na mimi nipate faraja lakini hawakuweza kufanya hivyo - Wolper
Hata hivyo Wolper amekiri wazi hata tatizo na Mhe Lowassa na hawezi kumlaumu kwa yaliyotokea bali atakuwa naye bega kwa bega tena kumsapoti endapo atapata tena nafasi ya kugombea urais 2020.
Mtazame hapa chini Wolper akifunguka kwa undani zaidi.