Utafiti mpya unaonyesha uhusiano kati ya unywaji wa pombe miongoni mwa wanawake na ongezeko la kupata na saratani ya matiti.
Kwa
mujibu wa ripoti kutoka na mfuko wa utafiti wa saratani ni kuwa nusu
glasi ya mvinyo au bia kwa siku inaongeza uwezekano wa kupata saratani
ya matiti.Pia utafiti unaonyesha kuwa mazoezi ya mara kw mara yanaweza kupunguza hatari ya kupata maradhi hayo.
Saratani ya matiti ndiyo huwakumba zaidi wanawake nchini Uingereza huku mmoja kati ya wanawake wanane wakipatwa na ugonjwa huo katika maisha yao.
Lakini wanasayasni wanasema kuwa hawawezi kueleza ni kwa nini watu wengine hupatwa na saratani na wengine hawapati.
Kuna sababu kadha ambazo zastahili kuangaliwa ikiwemo mtindo wa kuishi, viwango vya homoni na masuala mengine ya kiafya.
Kwanza kuna masuala kadha ambayo mtu hawezi kuyadhibiti kama vile jinsia, umri , kimo na mengineyo.
Kuwa mwanamke aliye na zaidi ya miaka 50 na aliye na historia ya ugonjwa wa saratani katika familia, inaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huo.
Kuwa na kimo kiferu na kuanza kupata hedhi kabla ya umri wa miaka 12 pia huongeza hatari
.
Taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza inasema kuwa kuna masuala ambayo yanaweza kuchangia ugonjwa wa saratani kwa kiwango fulani na pombe ni moja yao