Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea.
Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.
Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa
za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang.
Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu
mpango waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera.
Alikuwa awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi.