Kumbukumbu ya miaka 29 ya Bingwa wa Usomaji Qur'an Sheikh Abdul Basit

"NI  MIAKA 29 IMEPITA TANGU  KUFARIKI KWA BINGWA WA USOMAJI WA QURAN
   "Sheikh [Abdul-Bassit-Abdul-Samad]

            "WASIFU  WAKE"
      
"Msomaji bingwa wa Quran Sheikh Abdul-Bassit-Abdul-Samad  Mmoja wa waalimu Maarufu na qarii (Msomaji) Maarufu wa Quran.

"Abdul Bassit Alianza kujifunza Quran tukufu tangu akiwa mdogo na alipofikia umri wa miaka 11 Alifanikiwa kupata tuzo ya kuhifadhi na kusoma Quran.

"Sheikh Abdul-Bassit katika maisha yake alijishughulisha  na usomaji wa Quran tukufu na kutunikiwa zawadi na tuzo maalumu katika mashindano ya kimataifa ya Kusoma  Quran tukufu kwenye nchi za kiislamu. Na katika miaka ya 1970 alishinda mara 3 ubingwa wa usomaji wa Quran duniani (World qira`at Competitions)

Abdul-bassit Alikuwa na pumzi za ajabu katika usomaji wake, Ameacha kanda nyingi za sauti yake nzuri za usomaji Quran tukufu na ndiye mtu wa kwanza kurekodi Quran na kusambazwa sehemu mbalimbali.

"Abdul-Bassit Alizaliwa  mwaka 1927  katika kijiji kimoja huko Mji wa Armant kusini Mwa nchi ya Misri.
Baba yake alikuwa ni Mkurdi wa Iraq na Mama yake Mwarabu wa Misri. Mwaka 1950Alihamia mji wa cairo na waislamu wengi  walivutiwa na usomaji wake  na kuigwa na kila na kila msomaji.

"Abdul-Bassit amesafiri sehemu nyingi kwa  ajili ya usomaji wa Quran. Mwaka 1961 Alikwenda Pakistan na kusoma Quran katika Masjid Bad shashi huko lahore Mwaka 1987  Alikwenda  Amerika.
"Moja ya maajabu yake ya usomaji wake wa Quran yalitokea wakati aliposafiri na raisi wa Misri wa kipindi hicho Gamal Abdel Nazeral kuelekea Urusi. Aliombwa na viongozi wa soviet party asome Quran.

"Anaeleza Abdul-Bassit kwamba watu wanne katika kila watu watano walikuwa #wakilia wakati anasoma Quran ya #ALLAH  japo hawakuwa wanaelewani nini maana ya kinachosomwa. Abdul-Bassit alikuwa fundi zaidi wa sauti ya (Bayat) kiasi cha kuitwa yeye ndiye baba wa sauti hiyo #Abubayat.
"Mmoja wa  watu waliokuwa  wakiathiriwa na usomaji wake japo hakuwa Muislamu ni waziri mkuu wa zamani India, Indira Gandhi. Abdul-Bassit Alifariki siku ya jumatano ya Mwezi Novemba Mwaka1988 kwa ugonjwa wa Hepatitis. Aliacha watoto watatu ambao ni Yassir, Hisham na Tariq. Yassir ndio aliyefuata nyayo za Baba yake katika usomaji wa Quran.

"Yaa ALLAH tunakuomba umrehemu sheikh wetu uko alipo na umkinge na adhabu zako za kabri

      #Allahumah Aaaaaaamiyn Yaa Rabb

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post