Tetesi za soka Ulaya Jumanne 16.02.2021: Konsa, Mbappe, Gundogan, Lingard, Aarons, Medina

 


Kiungo wa kati wa West Ham na England Jesse Lingard amesema "hakupata fursa" akiwa Manchester United baada ya kurejea kwa mchezo wa soka kutokanana na kusitishwa kwasababu ya virusi vya corona. Mchezaji huyo, 28, yuko kwa mkopo Hammers hadi mwisho wa msimu. (BT Sport)

Liverpool, Manchester United, Manchester City na Tottenham zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Schalke raia wa Marekani Matthew Hoppe, 19. (90min)

Ezri Konsa
Maelezo ya picha,

Ezri Konsa

Liverpool inamfuatilia mlinzi wa Aston Villa Ezri Konsa, 23, huku wakifikiria kama inawezekana wamchukue mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa Under-21. (Athletic - subscription required)

Chelsea ndio klabu pekee ya Ligi ya Primia kutoa ofa ya mkataba kwa mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba. Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwisho wa msimu huu na yuko huru kufanya mazungumzo na klabu nyingine. (90min)

France's Kylian Mbappe
Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, ameiambia Paris St-Germain angependa kuangalia mkataba wake ambao unamalizika 2022. (Sport - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 30, anataka kuhamia kwenye usimamizi wa soka na kuwa siku zake za kucheza zimeisha. (Goal)

Steve Cooper

Crystal Palace imemchagua kocha wa Swansea Steve Cooper kama anayeweza kuchukua nafasi ya Roy Hodgson. (Sun)

Fainali za kombe la FA na Carabao zinaorodheshwa kama majaribio ya kurejea kwa mashabiki kabla ya matukio ya michezo msimu huu. (Times - subscription required)

Max Aarons
Maelezo ya picha,

Max Aarons

Norwich imeiambia Bayern Munich italazimika kulipa pauni milioni 30-35 ikiwa inataka kumsajili mlinzi Max Aarons, 21. (Sky Sports)

Southampton ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Angers raia wa Ufaransa Angelo Fulgini. Saints ilijitahidi kumsajili, 24, mnamo mwezi Januari. (Le10 Sport - in French)

Jamal Musiala scored for England Under-21s in a 5-0 win over Albania in November
Maelezo ya picha,

Jamal Musiala

Kiungo wa kati wa England wa Under-21 Jamal Musiala, 17, anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na Bayern Munich. (Guardian)

Bayern pia imejipanga kumsajili mlinzi wa Reading, 17, Omar Richards. (Kicker)

Facundo
Maelezo ya picha,

Lens Facundo

AC Milan inamnyatia beki wa kati mlinzi wa Lens Facundo Medina, 21, ambaye pia analengwa na Manchester United. (Mail)

Nahodha wa Tottenham Harry Kane amezungumza na rafiki zake pembeni kuwa kocha Jose Mourinho ambaye anapitia shinikizo kubwa ana muunga mkono. (Football Insider)




Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post