PAPY Tshishimbi, nahodha wa Klabu ya Yanga amesema kuwa iwapo hatapewa mkataba ndani ya klabu hiyo yupo tayari kuondoka na kurejea nyumbani.
Sarakasi za usajili wa Tshishimbi zimezidi kushika kasi ambapo leo Agosti 2, mkataba wake unabakisha siku 10 kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Simon Patric alisema kuwa mkataba wa nyota huyo utakamilika Agosti 12.
Katibu huyo alisema kuwa alimpa mkataba Tshishimbi mezani na kumtaka asaini ndani ya siku 14 akishindwa kusaini dili hilo basi aondoke.
Tshishimbi amesema:” Nimeskia yote ambayo katibu amesema, hakuna mtu
ambaye anaweza kufanya masuala ya mkataba akapeleka kwa vyombo vya
habari akasema kwamba Papy amepewa siku 14 ili asaini mkataba. Kwa kuwa
wao wameongea sawa ninakubai lakini kwa nini hajaongea na Papy?
“Wao wanaweza kuachana na Papy leo sawa, ninaweza kupata timu nyingine ndani ya Tanzania ama nikakosa timu hakuna tatizo kwani nyumbani nimeua? Hapana nitarejea nyumbani,” amesema Tshishimbi.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na Tshishimbi ili wakifika makubaliano aongeze mkataba mwingine.
"Tshishimbi ni mchezaji mzuri na kwa sasa bado tupo naye kwenye mazungumzo malengo yetu ni kuona kwamba anabaki ndani ya timu," amesema.
Tags
Michezo