Mwanamuziki Linah Sanga APATA Kigugumizi Kuhusu Bernard Morisson


Kumekuwa na tetesi zikimuhusu msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga "Ndege mnana" kwamba yupo kwenye mahusiano na mchezaji wa timu ya Simba ambaye ni Raia wa Ghana bwana Benard Morisson.


Sasa Kamera za EATV & EA Radio Digital zimekutana na msanii huyo ambaye amejibu kuhusu tuhuma hizo ambapo ukitazama kwenye video hapo chini alikuwa kama amepata mchecheto na kutaka kusita kuliongelea suala hilo.

"Benard Morisson ni rafiki yangu na shabiki yangu mkubwa na tulikutana Instagram, hata alivyokuja Bongo hakuniambia ila nilisikia story tu, kuna siku nilienda mahali kukutana na marafiki zangu wengine kuna mtu akanifuata kuniambia Morisson anakuita kwahiyo nikaenda nyumbani kwao nikamkuta yupo sebuleni wanacheza PS kisha tukapiga picha" amesema Linah 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post