HAJI MANARA AFUNGUKA JUU YA GOLI LA OFFSIDE


Mlalamiko na lawama zimeendelea kuibuliwa katika michezo ya vigogo Simba na Yanga katika Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu kutokana na aina ya magoli yanayofungwa.

Kesi  hizo zimekuwa nyingi kuelekea kwa klabu ya Simba, ambapo katika mchezo wa jana, Februari 4, Simba ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania huku bao la kwanza lililofungwa na John Bocco likionekana kulalamikiwa kuwa ni la kuotea.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amejitokeza na kuzungumzia suala hilo katika ukurasa wake wa Instagram, akiwajibu wanaolalamikia goli hilo.

"Kwa wale mnaolalamika kua simba wamefunga goli la offside mnatakiwa kufika vituo vya polisi kuandika maelezo.
Usisahau kuja na kitambulisho cha Nida"

Simba inaendelea kuongoza ligi kwa pointi 50 mpaka sasa, baada ya kucheza michezo 19 iliyocheza, nafasi ya pili ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 37 na Namungo FC katika nafasi ya tatu kwa pointi 31. Wapinzani wao Yanga wako nafasi ya nne kwa pinti 31, baada ya michezo 16.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post