ALLY SONSO AWAOMBA RADHI MASHABIKI WA YANGA


Beki wa timu ya Yanga SC, Ally Mtoni ''Sonso'' ameomba radhi kwa wanamichezo wote kwa kadi nyekudu aliyoipata jana kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Azam FC uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Ameeleza hayo kupitia kwenye urasa wake wa Instagram ambapo ''Naomba msamaha kwa wana mchezo wote kwa kadi niliyoipata siku ya jana na tukio nililofanya kwenye mchezo wetu vs Azam fc,kweli mchezo wa mpira ni  mchezo wa furaha na upendo kwa kuwa ni ajira ila changamoto za hapa na pale zipo,pia naomba msamaha kwa wachezaji, viongoz wangu wa @yangasc na pia hata wa @azamfcofficial na hata viongozi wenye dhamana na soka letu @tanfootball na sitaweza kuja rudia tukio la aina ile

Mchezo huo Yanga ilipoteza kwa kufungwa goli 1-0


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post