ROTIMI afunguka kuhusu penzi lake na Vannesa Mdee

Mwezi mmoja baada ya taarifa za Vanessa Mdee kutoka kimapenzi na Rotimi, hatimaye jana muigizaji na mwimbaji huyo amezungumza kwa mara ya kwanza.

Rotimi ambaye ana asili ya Nigeria amethibitisha penzi lake na Vee Money kwenye mahojiano na kituo cha Redio cha The Beat 99.9 FM cha Nigeria. Amesema "She's pretty, She's a beautiful singer, she's dope. She's from Tanzania." Kisha kumtaja kuwa ni @vanessamdee

Kwenye maongezi yake Rotimi amesema penzi lao lina miezi kadhaa tu na kwa mara ya kwanza walikutana kwenye tamasha la Essence ambalo lilifanyika New Orleans nchini Marekani mwezi Julai mwaka huu ambapo pia Vee alitumbuiza. Aliongeza kuwa yeye ndiye alianza kumfata na kumtongoza

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post