Jeshi la Polisi laua Majambazi wanne


Askari wa kikosi maalum wilayani Biharamulo Mkoani Kagera wakiwa katika doria maeneo ya barabara ya Ngazi Saba inayounganisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi wamewaua watu wanne wanaosadikika kuwa ni majambazi na kufanikiwa kupata siraha moja aina ya SMG na risasi saba waliyokuwa wakitumia.

“Wakati askari wakiwa katika doria waliona kundi la watu likikimbilia porini na ndipo waliwaamuru wasimame na watu hao walikataa na kuanza kuwarushia askari risasi na ndipo askari waliamua kujibu mapigo na kufanikiwa kuua majambazi wanne na kufanikiwa kupata siraha moja,” Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas amesema.

CP Sabas ameongeza kuwa, kwa operesheni inayoendeshwa Mkoa wa Kigoma Wilaya ya Kasulu wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 42 kwa makosa mbalimbali na kati ya hao 24 wanatuhumiwa kwa unyanganyi wa silaha.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post