Edo Kumwembe aeleza kocha anaestahili kuwa Yanga sio Zahera


Baada ya Yanga SC kupoteza kwa kufungwa kwa goli 2-1 dhidi ya Pyramids FC katika mchezo wa Play Off wa kuwania kucheza Makundi ya Kombe la Shirikisho katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, kila mtu ameanza kuzungumza mawazo yake, Edo Kumwembe ambaye ni mchambuzi wa masuala ya soka ametoa mtazamo wake kupitia ukurasa wake wa instagram na kueleza kocha anayedhani anastahili kuwa Yanga SC.
“Mapinduzi, Makame, Banka, Tshishimbi ni wachezaji maridadi individually..lakini Yanga washinde au wafungwe, huwa wanakimbizwa…haijulikani kocha anataka wacheze vipi”>>>Edo
“Jana walimtenga kabisa Sidney…msimu huu kocha wao alipaswa kuwa kocha na sio kufanya kazi za Mwenyekiti, Katibu, Msemaji wa kubishana na Haji Manara au kuwa Mweka Hazina..Kama ningekuwa mtu wa Yanga walihitaji kuwa na mtu kama Kim Poulsen”>>>Edo
Yanga sasa watahitaji kwenda Cairo kupata ushindi wa kuanzia 2-0 kama watatakakusonge mbele, vinginevyo Yanga watakuwa wanaaga mashindano hayo, hata hivyo kocha wao mkuu Mwinyi Zahera anahusishwa kufukuzwa na nafasi yake kupewa Hans van Pluijm au Kim Poulsen.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post