AFCON yampa kitu Manula

Anasema kwamba anaamini kila mchezaji aliyechaguliwa kwenye kikosi cha Stars ni muzri na amefanya vyema kwenye timu yake.

KIPA wa Simba na Taifa Stars, Aishi Manula amesema Fainali za Mataifa Afrika (Afcon), yamewafunza mambo mengi kama wachezaji wa ndani ambao waliokuwa kwenye kikosi hicho.
Manula anasema ili kikosi hicho kiwepo bora zaidi ni vyema wachezaji wengi wanaocheza ligi ya ndani watoke kucheza nje ya nchi ili kupata uzoefu wa michuano mikubwa ya kimataifa.
Anasema kwamba anaamini kila mchezaji aliyechaguliwa kwenye kikosi cha Stars ni muzri na amefanya vyema kwenye timu yake.
"Kuna umuhimu wa wachezaji wengi wa timu ya Taifa kwenda kucheza ligi yenye ushindani na hata ambao tupo katika ligi ya ndani inabidi iongezwe ushindani ili wote tukikutana Stars tuweze kushindana na wachezaji wa aina hiyo,"
"Ukiangalia wachezaji tuliokutana nao katika mechi zetu tatu za makundi muda mwingi tulionekana tunacheza sawa lakini kuna vitu vidogo vidogo ambavyo wanatuzidi kutokana na kucheza ligi zao zenye ushindani mkubwa.
"Tumekutana na wachezaji wenye uzoefu wa mashindano hayo lakini hata ligi na timu zao za klabu wamecheza mechi nyingi zenye maandalizi makubwa na kuwapa uzoefu ambao wakifika kwenye mashindano kama hayo ya Afcon wanakuwa tayari wamezoea," anasema Manula.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post