Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi, Azam FC wamefanikiwa kutinga hatua ya Fainali baada ya kuwabamiza wapinzani wao KMKM mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa leo kwenye uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.
Ushindi wa mapema ulifanikiwa kuwachanganya wapinzani mara baada ya Agrey Moris kuandika bao la kwanza dakika ya tisa na kuwapeleka mapumziko Azam FC wakiwa kifua mbele kwa bao hilo.
Kipindi cha pili Azam FC walifanikiwa kuandika bao la pili dakika ya 62 kupitia kwa Salum Abubakari 'Sure boy' na Obrey Chirwa akamalizia msumari wa mwisho dakika ya 81
Kwa ushindi huo Azam FC wanasubiri mpinzani wao watakaecheza nae fainali ambaye atakuwa mshindi kati ya Simba na Malindi ambao wataingia Uwanjani saa 2:15 usiku, fainali itachezwa Januari 13.
Tags
MAPINDUZI CUP