Msanii wa muziki wa bongo fleva na kipenzi cha wengi, Ali Kiba, ameweka wazi kilichokatisha ndoto yake ya kuwa na elimu kubwa, na kumfanya hata elimu ya sekondari asimalize.
Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Television, Alikiba amesema familia yake ndio chazo kikubwa cha kutomaliza kwake elimu ya sekondari, kwani haikuwa na uwezo wa kumlipia ada.
“Sikwenda form six wala form four sikumaliza, sikuweza kumaliza kwa sababu ya maisha ambayo nilikuwa naishi na familia yangu”, amesema Alikiba.
Hivi sasa Alikiba ni mmoja ya wasanii wakubwa Bongo na mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa, na mfano kwa vijana wengi nchini Tanzania.
Tags
WASANII