YAYA TOURE APATA TIMU MPYA




Wakala wa Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure, Dimitary Seluk, amesema mteja wake amefaulu vipimo vya afya jijini London na anakaribia kujiunga na klabu moja katika jijini humo.

Toure mwenye umri wa miaka 35 amekuwa mchezaji huru tangu mkataba wake na klabu ya Manchester City kumalizika msimu uliopita.

Toure kwa kipindi hicho chote amekuwa hana timu na wakala wake amekuwa akipambana kumtafutia timu kutokana na umri wake kuruhusu kucheza.

Mambo sasa yameonekana kuiva baada ya timu hiyo kupatikana lakini Seluk ameshindwa kuiweka hadharani mpaka pale mambo yatakapaoiva kwa asilimia 100.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post