Inasikitisha Ommy Dimpozi Afunguka Alivyotobolewa Tumbo na Kutolewa Lita Moja ya Usaha


Inasikitisha Ommy Dimpozi Afunguka Alivyotobolewa Tumbo na Kutolewa Lita Moja ya Usaha

Msanii wa muziki, Ommy Dimpoz bado yupo nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa baada ya kupata matatizo katika mfumo wake wa kumeza chakula na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuubadilisha mfumo huo.

Akizungumza na Millardayo nchini Afrika Kusini, Ommy Dimpoz ameweza kusimulia namna upasuaji wake ulivyofanyika na kusababisha kukaa Chumba cha Uangalizi Maalumu ICU kwa muda wa wiki tatu baada ya mapafu yake kuleta shida.

"Sijui sumu iliingia lini na ikifika part ya kusungumzia sumu napata tabu sana na huwa sipendi sana kuzungumzia ila kwasasa nimepungua kilo ishirini ambapo nilifanya mazoezi jim kwa miaka miwili nilipoteza kilo mbili" alisema Ommy Dimpoz

Kuhusu sumu sijii nani kaniwekea wala siwezi nikamuhisi mtu yoyote kuwa anaweza kuniwekea ila kila mtu ana maaduhi na siwezi nikajua kama nani ni adui yangu

Ommy Dimpoz ameendelea kusema kuwa amerudi tena sauz si kama taarifa zilivyokuwa zinasambazwa mitandaoni kuwa hali yake mbaya sana bali ameenda kwakuwa alipewa miezi mitati kwaajili ya kuangaliwa maendeleo yake  baada ya kufanyiwa oparesheni kubwa na inawezekana nikaambiwa nirudi tena siku yoyote.

"Baada ya Kurudi hospitali tena nikawaelezea hali yangu iivyo walinifanyia vipimo tena ila waligundua nina usaha mwingi sana wakanambia inabidi wanitoboe pepeni ya tumbo ili unyonywe ila siku ya kwanza walitoa lita moja nzima ya usaha"

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post