YANGA YAJIBU MAPIGO SIMBA, NYOTA WAWILI WAMWAGA WINO KWA MPIGO, WAWILI WANAFUATA



Mabingwa wa kihistoria katika soka la Bongo, Yanga, imeanza kujibu kujibu mapigo ya watani zao wa jadi Simba kwa kunasa saini mpya za wachezaji wawili.

Wachezaji hao ni beki wa kulia Juma Abdul ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea klabu hiyo na kuzima ndoto za kuelekea Azam kama ambavyo awali ilikuwa ikitajwa.

Abdul aliingia katika tetesi za kuhusishwa kutua Azam lakini mabosi wa Yanga kupitia Kamati ya Usajili imejitahidi kuwapiga kete matajiri hao na kumalizana naye kwa kumuongezea mwaka mmoja.

Mbali na Abdul, Yanga imefanikiwa kumrejesha kiungo wake mjanja Deus Kaseka ambaye waliwahi kumsajili akitokea Mbeya City na baadaye kutimkia Singida United ya Singida.

Kaseke amerejea Yanga na kusaini kandarasi ya mwaka mmoja pia sawa na Abdul ambaye ameongeza muda huo katika harakati za kujiandaa kuelekea msimu ujao wa ligi.

Taarifa za ndani kutoka Yanga ukiachana na Abdul pamoja na Kaseke, inaelezwa Kamati ya Usajili ipo kwenye mazungumzo na beki Andrew Vincent pamoja na kipa Beno kakolanya kwa ajili ya kusaini kandarasi mpya na muda wowote wanaweza wakamwaga wino.

1 Comments

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post