Argentina wamekalia kuti kavu World Cup 2018


Timu ya taifa ya Argentina usiku wa June 21 2018 ilicheza game yake ya pili ya Kundi D katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Croatia katika uwanja wa Nizhny Novgorod.

Argentina ambao awali walitoka sare dhidi ya Iceland kwa kufungana goli 1-1, leo wamekutana na kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Croatia, mfumo wa kujihami zaidi umeisaidia Croatia kabla ya kutumia vyema uzembe wa golikipa wa Argentina Wilfredo Caballero kuchopu mpira aliyokuwa karudishiwa na beki wake na hatimae kuishia miguu mwa Ante Rebic na kufunga dakika ya 53.

Baada ya Argentina kuruhusu goli la kwanza umakini ulizidi kupungua zaidi kutokana na kuzidi kupata presha na kujikuta dakika ya 80 nahodha wa Croatia Luka Modric anafunga goli la pili kabla ya Ivan Rakitic kufunga goli la mwisho dakika za nyongeza kabla ya game kuisha.

Kipigo hicho kimewaweka pabaya zaidi Argentina na kufanya kuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele World Cup 2018, kwani matokeo ya game kati ya Nigeria na Iceland itatoa picha halisi ya nani ana nafasi lakini kwa sasa Argentina anapaswa kuomba apate ushindi mnono dhidi ya Nigeria kwani ana point moja pekee.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post