YANGA YAFUNGA LIGI KWA KIPIGO


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2017/2018 imemalizika kwa michezo 15 kucheza leo Jumatatu ya May 28 2018 katika viwanja mbalimbali Tanzania, Yanga walikuwa uwanja wa Taifa Dar es kucheza mchezo wao wa mwisho wa Ligi dhidi ya Azam FC.
Yanga leo wamekutana na kipigo cha magoli 3-1 kutoka Azam FC magoli ya Azam FC yakifungwa na Yahaya Zayd dakika ya 4, Shaban Iddi dakika ya 60 na Salum Abubakar dakika ya 68 wakati goli pekee la Yanga lilifungwa na Abdallah Kheri wa Azam FC aliyejifunga.
Kipigo hicho sasa kinaifanya Yanga kumaliza Ligi wakiwa nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC waliyopo nafasi ya pili, wakati club ya Majimaji ya Songea baada ya kutoa sare ya 1-1 na Simba wanaungana na Njombe Mji kushuka daraja.
Msimu wa 2018/2019 Ligi Kuu itakuwa na jumla ya timu 20 ambapo timu za Biashara ya Musoma, Coastal Union ya Tanga, KMC ya Kinondoni, Alliance ya Mwanza, JKT Tanzania na African Lyon ambapo timu hizo zimepanda daraja kucheza Ligi Kuu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post