Wakati Yanga ikiwa katika harakati za kujiandaa na uchaguzi wa kumpata Mwenyiki wa klabu hiyo, Mjumbe na Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali ameibuka akiitaka nafasi hiyo.
Akilimali ameweka wazi nia ya kugombea nafasi hiyo iliyokosa mtu kwa muda mrefu tangu Yusuph Manji atangaze kujiuzulu alipoomba kupumzika.
Mzee Akilimali ameeleza kuwa Yanga inapitia wakati mgumu kwa sasa hivyo ni vema akapata nafasi ya kugombea kiti hicho akisema ataweza kuikwamua kwenye matatizo iliyonayo.
Kutokana na hali hiyo Akilimali amedai ni wakati mwafaka sasa kwa Yanga kutoka katika hali waliyonayo ya kuyumba kiuchumi ili warejee kama zamani walivyokuwa katika hali nzuri.