Huku kikosi cha Yanga kikitarajia kushuka uwanjani leo usiku kupambana na Azam FC, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeiruhusu klabu hiyo kumtumia beki wa kati, Kelvn Yondani katika mechi hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yondani alikuwa nje ya uwanja bila ya kuitumikia timu hiyo baada ya kumusimamisha na TFF kwa kosa la kumtemea mate beki wa kushoto wa Simba, Asante Kwasi na tayari alikuwa ameshakosa mechi tano.
TFF kupitia kwa kamati yake ya masaa 72 ndiyo iliyotoa uamuzi huo wa kumsimamisha Yondani kuitumikia timu yake hiyo mpaka hapo suala hilo litakapojadiliwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutoka na kosa hilo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa leo hii saa 5:00 mchana wamepokea barua kutoka TFF ikiwaruhusu kumutumia Yondoni katika mchezo huo dhidi ya Azam FC.
“Hata hivyo, barua hiyo hajasema chochote kuhusiana na adhabu ila imetupatia ruhusa ya kumutumia katika mechi yetu ya leo na Azam FC,” amesema Mkwasa.