Vilio Vyatanda Baada ya Kumpata Mtoto Wao Aliyepotea kwa Miaka 24


Familia moja nchini China imeibua hisia nyingi za watu baada ya kumpata mtoto wao wa kike ambaye alikuwa amepotea kwa miaka 24.

Inaelezwa kuwa binti huyo  Qifeng alipotea akiwa na umri mdogo, ambapo siku moja akiwa na wazazi wake Wang Mingqing na Liu Dengying ambao walikuwa wauzaji wa matunda, alipotea na wazazi hao waligundua mtoto wao hayupo pembeni yao.

Walianza kumtafuta, zoezi ambalo lilichukua miaka hiyo yote huku wakitangaza kumtafuta binti yao huyo kwenye vyombo mbalimbali za habari nchini humo huku baadhi ya mabinti wakijitokeza kupiga DNA lakini hawakuwa mtoto wao.

Hatimaye Polisi mchoraji alichukua picha ya utotoni ya binti huyo na kumchora jinsi ambavyo yawezekana ndivyo alivyo baada ya kuwa mtu mzima. Qifeng alipoona picha hiyo alipiga simu kwa namba ambazo ziliwekwa kwenye picha hizo na ndipo wanafamilia hao walipopatana.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post