Ipo Siku Watu Watajua Nastahili au Sistahili Kuwa WCB- Mbosso

Msanii wa muziki Bongo, Mbosso amesema kitafikia kipindi watu watajua ni kwanini yeye yupo katika label ya WCB.

Muimbaji huyo amesema hayo kutokana na baadhi ya watu kukosoa kile anachokifanya licha ya kukiwasilisha katika njia iliyonzuri.

“Kuna muda unaweza ukafanya kitu kwako wewe kipo sawa na unajaribu kukiwakilisha kwa njia iliyo sawa lakini inafikia hatua anaona hakiko sawa anafikia hatua hata ya kukutukana matusi, inafikia hatua mtu anakutukana mpaka matusi ya mama yako,” Mbosso ameiambia TBC FM.

“Lakini huwezi kumzuia mtu kufanya hivyo vitu ila kuna muda utafiki kila mtu atajua Mbosso kumbe anastahili kuwa WCB au anastahili kupewa hiki ambacho anapewa sasa hivi,” ameongeza.

Mbosso ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Picha Yake, alitangazwa rasmi kuwa chini ya WCB January 28 mwaka huu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post