Endapo Yanga SC itafanikiwa kuwatoa Dicha itaingiza kiasi hiki cha fedha kutoka CAF


Jana Aprili 08, 2018 klabu ya Yanga imefanikiwa kupata matokeo ya goli 2-0 dhidi ya Waethiopia ‘Welaytta Dicha’ kwenye mchezo wa kombe la shirikisho Afrika, ambapo kwa sasa Yanga watahitaji ushindi au sare ya namna yoyote ili iweze kusonga mbele.

Endapo Yanga watafanikiwa kusonga mbele watajishindia kitita cha dola $150,000 sawa na tsh milioni 339 zinazotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kila klabu inayofanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Hata hivyo, Yanga SC wanaonekana kuwa imara zaidi na kutoa matumaini kwa Watanzania kwani licha ya mchezo wa jana kukosekana kwa wachezaji wao muhimu kama Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa na Said Juma ‘Makapu’ wanaotumikia adhabu ya kadi mbili za njano, bado Yanga wanaonekana kuwazidi uwezo Waethiopia hao.

klabu ya Yanga mchezo wa jana umekuwa mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika, baada ya kungolewaa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na klabu ya Township Rollers ya Botswana.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post