Uchebe Afunguka "Sijawahi Mzibua Shilole Toka Nimuoe

MUME wa staa wa Mduara Bong , Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambaye alifunga naye ndoa miezi kadhaa iliyopita, Ashiraf Uchebe amefunguka kuwa, tangu aingie kwenye u husiano na mwanamama huyo hadi sasa , hajawahi hata kumzibua kofi.

 Uchebe aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, watu wengi wanamuona yeye kama baunsa ambaye kila wakati anaweza kupiga mtu, jambo ambalo si kweli kwani anampenda mno mkewe huyo hivyo hawezi kumtandika makofi.

 “Watu wengi wananiona kama mtu wa kupigapiga, lakini siwezi kumtandika mke wangu hata siku moja,” alisema Uchebe mwenye umbo dogo ukilinganisha na Shilole.

Kwa upande wake Shilole alipoulizwa kuhusu habari zilizoenea mitandaoni za kupokea kipondo kutoka kwa Uchebe alisema hakuna ishu kama hiyo.

IMELDA MTEMA, DAR

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post