TFF Yafunguka Baada ya Kupokea Ombi la CECAFA


Kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupokea barua kutoka Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ikiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya KAGAME, TFF wamesema watafikiria ombi hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario, amesema kuwa ni kweli wamepokea barua hiyo, ila watakaa wajadili kama taasisi ili baadaye waweze kuja na majibu rasmi ya michuano hiyo kama itafanyika au kutofanyika.

Clifford ameeleza kuwa watahitaji kufikiria ombi hilo kulingana na hivi sasa ina ratiba ya mashindano ya soka la vijana kuelekea kufuzu AFCON chini ya miaka 20, hivyo watakuja na jibu rasmi baadaye.

CECAFA imetuma barua hiyo ikiiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame kwa ngazi ya klabu ambayo yanataraji kuanza mwezi Juni 2018.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post