Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph haule maarufu kama Prof. Jay, amesema kwamba ameamua kuwasamehe wasanii ambao walimsaliti wakati wa kampeni za yeye kuingia Bungeni, kwa kujitol.
Prof. Jay amesema kwamba ameamua kufanya hivyo kwani ameona ni jinsi gani wasanii wamekuwa hawana umoja, hivyo sio vema kwa yeye kuwabagua kwa itikadi za vyama japokuwa walimpinga wakati wa kampeni za ubunge, kwa kuwa wanahitaji umoja ulio thabiti kwa ajili ya maslahi yao.
Prof. Jay ameendelea kwa kusema kwamba matatizo mengi wasanii yanawakuta kwa kuwa hawana umoja thabiti, huku wengine wakiwa na ubinafsi, hivyo ni jambo ambalo linatakiwa kukomeshwa kwa manufa yao wenyewe.
Tags
kitaifa