Hatimaye mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ameanza kufanya mazoezi na klabu yake mpya ya LA Galaxy ya Marekani.
Ibrahimovic (36) ambaye amekabiziwa jezi namba tisa, alikubali kujiunga na timu hiyo wiki iliyopita kwa mkataba wa miezi 18.
Mchezaji wakati akiongea kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, amesema alitaka kujiunga na LA Galaxy tangu mwaka 2016 wakati alipomaliza mkataba wake na PSG lakini dili hilo lilibadilika na kutimkia Manchester United.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA