Mwanamuziki Mimi Mars amefunguka aina ya mwanaume ambaye ni vigumu kuwa naye katika mahusiano.
Hitmaker huyo wa ngoma ‘Sitamani’ ameiambia Bongo5 kuwa ni vigumu kutoka na mtu wa kabila lake, “Kabila, sijawahi waza hilo suala, nahisi Mpare mwenzangu, sitokaa nijaribu hilo,” amesema.
“Tabia zetu kidogo, sasa wote tukikaa wawili kule ndani, kwanza hatutoendani ni ile wanasema mafahali wawili hawakai zizi moja,” amesisitiza.
Mimi Mars kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Papara, huu ni wimbo wake nne kuachia official baada ya Sugar, Dedee na Sitamani.