Meneja Atiwa Mbaroni .....Amwingiza Irene Uwoya Matatani



MSANII wa fi lamu Bongo, Irene Uwoya ameingia matatizoni baada ya meneja wake wa bar iliyopo Sinza, Mariam Ismail ‘Mamakubwa’ kuwekwa mahabusu polisi kwa sababu ya kukiuka sheria ya vileo kwa kuuza vinywaji nje ya muda ulioelekezwa na serikali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu tukio hilo lilijiri siku ya Jumatatu majira ya saa nane kasoro usiku, ambapo bar hiyo ilikuwa wazi ikiendelea na shughuli zake kama kawaida wakati kisheria inapaswa ifungwe saa tano usiku, ndipo askari wa doria wakamnasa meneja wake huyo.

“Inasemekana hiyo bar huwa inachelewa kufungwa mara kwa mara, sasa vyanzo vilivyopo jirani na eneo hilo vikatoa taarifa kwamba inakuwaje bar hiyo ifanye shughuli zake kinyume na sheria, nadhani ndiyo maana askari hao wa doria wakaweza kufi ka hapo.

“Hata hivyo, hawakumkuta Uwoya, ikabidi wamchukue huyo meneja wake ambaye naye ni msanii, walichukua viti kadhaa vya bar kama ushahidi, akapelekwa Kituo cha Polisi mabatini (Kijitonyama), ambapo ndani ya muda mfupi wenzake walifi ka wakafanya harakati za kumtoa, akiwemo msanii wa siku nyingi Nora,”aliongeza mtoa habari.

Kufuatia ishu hiyo paparazi wetu alimvutia waya muhusika wa bar hiyo, Irene Uwoya ambaye alikana kuifahamu ishu hiyo na kusema kuwa:

“Mimi sifahamu chochote kuhusu kukamatwa kwa meneja wangu, wewe ndio unanijulisha maana ndio ninaamka na sikuwepo eneo la tukio, sijasafi ri ila sipo tu huko kazini.”

Kufuatia tukio hilo gazeti hili lilifuatilia Kituo cha Polisi Kijitonyama na kukuta kuna jalada la kesi limefunguliwa na kupewa namba KJN/RB/1749/2018 KUUZA POMBE BAADA YA MUDA KUISHA ambapo polisi mmoja alisema wanafanyia kazi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post