Jay-Z na Beyoncé wakiwa kwenye boda boda uswahilini


Kama ni mfuatiliaji wa wasanii wawili wa muziki kutoka nchini Marekani, Beyonce na Jay Z kuanzia jana kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na picha za mastaa hao zikisambaa kwa kasi zikiwaonesha wakiwa kwenye boda boda katika maeneo ya uswahilini.

 Watu wengi mwanzoni walidhani ni picha za kutengenezwa kutokana na hadhi ya wasanii hao, lakini ukweli ni kwamba picha hizo ni zao na ni za kweli.



Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail umeeleza kuwa picha hizo za wawili hao wamepiga nchini Jamaica kwenye utengenezaji wa scene ya ziara yao ya kimuziki ya OTR II.

Kwa upande mwingine, mbali ya kutangaza tour yao ya pamoja kwa mara ya pili kuna tetesi kuwa wawili hao huenda wakaachia albamu ya pamoja siku za usoni.


Ziara hiyo ya On The Run II (OTR II) itaanzia katika mji wa Cardiff nchini Uingereza ifikapo Juni 6, 2018 na kumalizika Oktoba 2, mwaka huu katika mji wa Vancouver, nchini Canada ambapo itazunguuka zaidi ya miji 35 duniani.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post