Rais wa FIFA awasili Jijini Dar

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani Gianni Infantino leo alajiri amewasili Dar es Salaam kwa ajili ya kongamano maalumu la kutathmini maendeleo ya mpira wa miguu (The Executive Football Summit) litakalofanyika leo Februari 22, 2018.

Baada ya kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, Infantino amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Michezo Yusuf Singo, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Leodger Tenga na Rais wa TFF Wallace Karia.

Baada ya Infantino kuingia kuchaguliwa Rais wa FIFA mwaka 2016, alipendekeza kufanya makongamano yatakayofahamika kama The Executive Football Summits na yatafanyika kwa mfumo mfuatano (series).

Makongamano haya ni moja ya jitihada za msingi za Infantino kuleta mabadiliko ndani ya FIFA kwa kutoa jukwaa la kubadilishana mawazo na uzoefu sambamba na kuongeza ushirikishwaji wa wanachama wote wa FIFA katika maamuzi ya kimkakati ya shirikisho hilo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post