Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar



Marubani wawili wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya ndege iliyotokea Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar walipokuwa wakiifanyia majaribio ya kuruka wakati wa matengenezo.

Marubani hao wametajwa kuwa ni injinia Edger Alfred Mcha (26) na Dominic Bomani (64).

Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Tropical Air, David Kisusi amesema ndege hiyo ilianguka na kuungua jana, Alhamisi Februari Mosi saa saba mchana.

Kisusi amesema ndege hiyo 5H-TDF yenye uwezo wa kubeba abiria wanne ni mali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) iliyokuwa Zanzibar kwa matengenezo.

Amesema kwa takriban miezi sita ndege hiyo ilikuwa uwanjani hapo kwa matengenezo.

“Tulikuwa tunaijaribu baada ya matengenezo, iliporuka tu ilianguka na kulipuka, marubani wetu wamefariki dunia,” amesema Kisusi leo Februari 2, 2018.

Daktari bingwa wa uchunguzi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk Msafiri Marijani amesema vifo vya marubani hao vimesababishwa na kukosa hewa safi wakati wa ajali na kuathiriwa na moto.

Amesema uchunguzi wa miili ya marubani hao uliofanywa jana saa 12:45 jioni. 


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post