Infantino ametaja sababu FIFA kuchagua kufanya mkutano Tanzania

Inawezekana ujio wa Rais wa FIFA gianni ifantino nchini pamoja na wajumbe mbalimbali wa shirikisho hilo la soka duniani umestua watu wengi ambao wanajiuliza kwa nini wamechagua kuja Tanzania halafu wanakosa majibu.

Infantino amesema wamekuja Tanzania kwa sababu shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA si la baadhi ya mabara wala baadhi ya nchi huko barani Ulaya bali ni shirikisho ambalo linaongoza nchi nyingi ambazo ni wanachama na kuja kwao nchini ni kuonesha namna ambacho wanajali kila nchi mwanachama.

Amesisitiza pia wamegundua mambo mengi baada ya mkutano wao ikiwa ni pamoja na namna ambavyo mkutano wao umefanikiwa, kuzidisha uhusiano kati ya FIFA na TFF na wanachama wengine wa FIFA.

“Kwa upande wangu kama Rais ni kuishi ambacho tunakisema kwamba FIFA ni shirikisho la mpira wa miguu duniani, hatuwezi kuendesha FIFA duniani kote wakati tunajifungia sehemu moja ni lazima tutoke kwenda kwa wadau wetu ambao ni vyama wanachama ambapo Tanzania ni miongoni mwao na kwa sababu hiyo ndiyo maana tupo hapa.”

“Kongamano lililofanyika hapa ni muhimu kwa sababu tumekutana na wawakilishi kutoka mabara mbalimbali (Asia, America ya Kati na Kaskazini, Caribean na Afrika) kwa ajili ya kujadili kuhusu maendeleo ya soka duniani ikiwemo mashindano ya soka la vijana na wanawake ambayo kwa kiasi kikubwa yamesahaulika.”

“Ni muhimu kuja huku kwa sababu ni miongoni mwa maeneo ambayo yalisahaulika na fifa, tumeamua kuja Tanzania hususan Dar es Salaam angalau kwa siku moja na kufanya shughuli rasmi ya kiofisi.”

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post