Baada ya Mama Samia Kuvutiwa na Caver ya Subalkheri Awaalika Aslay na Nandy Nyumbani Kwake

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwakaribisha nyumbani kwake wasanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ na Faustina Charles maarufu kama Nandy kwa ajili ya mazungumzo mafupi na chakula cha jioni.

Katika mazungumzo yake na wasanii hao, Bi Samia alieleza kuvutiwa sana na marudio ya kibao cha SUBALKHERI kilichorudiwa na wakali hao wa Bongo Fleva hivi karibuni na kuwapa wosia wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi na kujiepusha na makundi mabaya. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post