Arsene Wenger anafukuzia rekodi ya kuwa kocha wa 8 kufanya jambo hili


Hivi unajua kwamba tangu mzee Arsene Wenger aichukue Arsenal mwaka 1996 hajawahi kuchukua kikombe cha ligi? Tangu wakati inaitwa Carling Cup hadi sasa inaitwa Carbao Cup  Wenger hajabeba.

Mwaka 2011 mashabiki wengi wa Arsenal waliamini kwamba ni wakati wao kuchukua kombe hilo baada ya kuingia fainali na timu dhaifu ya Burmigham lakini Gunners waliishia kupigwa 2-1.

Kwa mara ya kwanza siku ya Jumapili kocha Arsene Wenger anapewa nafasi kubeba kombe hilo kwa mara ya kwanza watakapokutana na Man City lakini pia ni nafasi kwa Pep Gurdiola kuchukua kombe

Ukiacha hilo lakini mchezo huu wa Carbao Cup unaweza kumfanya kocha Arsene Wenger kuwa kocha wa 8 katika historia ya nchini Uingereza kushinda makombe yote matatu ya ndani katika nchi hiyo (EPL, FA na Carbao Cup).

Sir Alex Ferguson anaongoza orodha ya makocha waliochukua makombe hayo mara nyingi hadi sasa akiwa ameshachukua EPL mara 13, FA mara 5 na kikombe cha ligi mara 4 akifuatiwa na Kenny Danglish aliyechukua EPL mara 3, FA mbili na kombe 1 la ligi.

Jose Mourinho, kocha wa sasa wa Manchester United naye pia amechukua yote matatu akichukua EPL mara 3, akaja akabeba FA mara 1 na kisha vikombe 3 vya ligi.

George Graham, huyu alikuwa kocha wa Arsenal kabla ya Wenger na akafanikiwa kushinda nao makombe mawili ya EPL, Graham alishinda pia FA mara moja na vile vile akashinda vikombe vya ligi mara tatu.

Bill Nicholson, msimu wa mwaka 1960/1961 Tottenham walishinda makombe mawili kwa mpigo, walibeba FA na kikombe cha ligi na mwalimu wao alikuwa Nicholson, 1973 alikamilisha kwa kushinda EPL akiwa na Aston Villa.

Pia kocha wa zamani wa Leeds Don Revie alifanikiwa kubeba makombe yote hayo matatu  na Joe Mercer ambaye naye alikuwa kocha wa zamani wa Manchester City nao walifanikiwa kufanya hivyo.

1 Comments

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post