Yanga imechukua pointi 28 kwa Azam


Ushindi wa Yanga dhidi ya Azam umeifanya Yanga kuchukua jumla ya pointi 28 kwa Azam tangu timu hizo zimeanza kukutana kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara.

Timu hizo zimekutana mara 19 kwenye michezo ya ligi kuu, Yanga imeshinda mara saba (7) sawa na pointi 21, zimetoka sare katika michezo saba (7) ambayo ni sawa na pointi saba hivyo kufanya jumla ya pointi 28.

Azam wameshinda mechi tano za ligi dhidi ya Yanga tangu wakutane kwa mara ya kwanza msimu wa Oktoba 15, 2008.

Yanga ikiwa ugenini imeibana Azam na kuichapa kwa mabao 2-1 ushindi ambao umeipa Yanga pointi tatu na kuifanya ifikishe pointi 28 na kubaki nafasi tatu ikiwa ni tofauti ya pointi mbili na Azam ambayo ina pointi 30 katika nafasi ya pili huku ikiwa nyuma ya Simba kwa pointi nne.

Ushundi wa Yanga umekuja wakati timu hiyo ikikabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye majeraha (Yohana Mkomola, Pato Ngonyani, Thabani Kamusoko, Amis Tambwe, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Pius Buswita ambaye alikuwa anatumikia kadi tatu za njano).

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post