Na Geza
Sio jambo la kushangaza Mesut Ozil kuongeza mkataba. Ozil alikuwa na nafasi kubwa ya kuondoka dirisha dogo. Lakini kufikia sasa ni ngumu kuondoka tena. Zipo sababu ambazo kwa mtazamo wangu mimi zinamfanya asiondoke.
Dili la Sanchez
Mourinho alitaka kumpeleka Ozil Old Trafford. Ozil aliwahi kufanya kazi na Jose Mourinho wakiwa wote ndani ya klabu ya Real Madrid. Dili la Sanchez kwenda Uninted limetibua mipango. Sanchez alihitajika na Man city lakini amebadili gia angani. Man united haiwezi kumnasa tena Ozil na Sanchez kwa wakati mmoja, ni sawa na Magu na JK kwenda UKAWA wote kwa pamoja. Bila shaka Wenger hawezi kumuozesha mwanae wa kike pia akampa na mkwe Ng’ombe badala ya yeye kupokea mahari (Mkhitaryan).
Ujio wa Majina mapya
Hii ni Kamari kwa Mesut Ozil. Wenger amethibitisha ujio wa majina mapya. Arsenal inaweza isipate mafanikio makubwa lakini bado wana nafasi ya kushiriki michuano mikubwa na midogo. Malcom raia kutoka Brazil, Piere Aubemeyang kutoka Borussia Dotmund pamoja na Henrik Mkhitaryan kutoka Manchester United ni majina yaaliyopo kwenye notibuku ya wenger. Kwa akili ya haraka haraka kikosi cha arsenal kitaimarika sana hasa baada ya Chamberlain, walcot pamoja na sanchez kuondoka. Bali hiku litampa hamasa mpya Mesut Ozil kubaki.
Haoni pakwenda na hahitajiki sana
Ozil ni mchezaji wa kiwango cha juu. Ni moja kati ya viungo mahiri sana katika robo ya eneo la timu pinzani. Shida ni kasi yake ya uchezaji. Ni makocha wachache wanaoweza kumvumilia.
Ni mchezaji ambaye tayari ameshacheza klabu kubwa kama Real Madrid. Mbaya Zaidi katika umri wake wa miaka 29 bado yupo kwenye kiwango salama. Ana kiwango bora bado, lakini ni timu gani ipo tayari kutoa ada ya kumnunua na kumlipa maslahi anayotaka katika umri wake huu? Ozil anafahamu fika kiwango chake bado hakijshuka, na anahitaji timu itakayokidhi maslahi yake. Je ni vilabu vingapi ambavyo vinaweza kumlipa? labda avuke bara aende uchinani au Marekani. Je katika hivo vilabu vinavyoweza kumlipa kuna uhakika wa nafasi? Je vinahitaji huduma yake?. Kwa haraka haraka timu nazoziona ni kama PSG, Man United Man City, Barca na Buyern. Lakini wote hao wana wachezaji sahihi kwenye eneo Ozil analocheza.
Mimi nadhani Ozil anapaswa kumlaumu Sanchez aliyeenda kuchukua nafasi yake Old traford. Amepokonywa tonge hivyo apambane na sahani yake akomboleze mchuzi alioacha sanchez. Na Uzuri ni kwamba Muonekano wa Ozil n mpole, nadhani Wenger hashindwi kumbebeleza na akabaki