Mwanasayansi wa safari za anga za juu raia wa Marekani John Young ambaye alisafiri kwenda mwezi mara mbili na kuhudumu kama kamanda ya chombo cha kwazza cha safari za anga za juu amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.
Young alikuwa mtu pekee kuwai kushiriki safari za anga za juu za Gemini, Apollo na Space Shuttle.
Wakati mmoja pia alipata umaarufu kwa kusafirisha kisiri nyama kwenda safari ya anga za juu kwa mwnsasayansi mwenzake kama zawadi.
Young alistaafu mwaka 2004 baada ya taaluma ya miaka 42. Nasa wanasema kuwa alifariki siku ya Ijumma kutokana na ugonjwa wa kichomi.
Baada ya kuzaliwa huko San Francisco mwaka 1930 alipata shahada ya uandisi kutoka taasisi ya Georgia Institute of Technology na baadaye kuhudumu kama rubani wa jeshi la wanamaji wa Marekani.
Alijiunga na Nasa mwaka 1992 na mara ya kwanza kusafiri kwenda anga za juu mwaka 1965 wakati wa safari ya Gemini 3.
Mwezi Mei mwaka 1969 Young alikuwa miongoni mwa wanasayasansi waliosafiri kwa chombo cha Apollo 10 kama jaribio la safari ya kwenda mwezini kwa chombo cha Apollo 11 miezi miwili baadaye
Young baadaye alitembea kwa miguu mwezini mwaka 1972 kama kamanda wa safari ya Apollo 16.
Tags
Teknolojia