Msimamo wa Ronaldo ndani ya Madrid

Nyota wa mabingwa wa ligi kuu ya Hispania Real Madrid Cristiano Ronaldo, amesema ana mapenzi makubwa na klabu hiyo hivyo tetesi za yeye kuondoka si za kweli na wala hana mpango wa kuondoka Bernabeu.

Ronaldo ameyasema hayo leo kuelekea mchezo wa La Liga kati ya timu yake dhidi ya Valencia utakaopigwa jioni hii majira ya saa 12:15. Na hii imekuja baada ya kuwepo kwa tetesi za kutaka kutimkia PSG au Manchester United.

"Naomba kuwatoa shaka mashabiki kuwa naipenda hii klabu na ninapenda kubaki hapa  pia napenda kuishi hapa sehemu ambayo nimekuwepo tangu 2009'', amesema.

Msimu huu Ronaldo hajaanza vizuri ambapo hadi sasa amefunga mabao sita pekee kwenye ligi huku mabingwa hao watetezi wakiwa na alama 35 katika nafasi ya nne wakizidiwa alama 19 na vinara Barcelona wenye alama 54.

Ronaldo mwenye miaka 32 ana mkataba na Real Madrid hadi 2021. Kwa upande wa umri wake amesema bado ana nguvu ya kutosha ya kucheza kwa muda mrefu kadri atakavyoweza.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post