Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mdogo wa msanii Vanessa Mdee, amefunguka tuhuma za kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Rapper Joh Makini
Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Mimi Mars amesema yeye na Joh Makini ni sawa na mtu na kaka yake, kwani Joh Makini alikuwa rafiki kipenzi wa kaka yake.
“Mahusiano yangu mimi na Joh Makini ni ya kidada na kaka, kwa sababu Joh Makini ni mtu ambaye tumemjua kuanzia tukiwa wadogo, alikuwa rafiki yake kaka yangu mkubwa, kwa hiyo kama ambavyo kaka yetu mkubwa anatushauri ni sawa na Joh Makini, ni rafiki, ni kaka, ni mshauri, sijui suala la mahusiano limetoka wapi”, amesema Mimi Mars.
Mimi Mars amesema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote akikusuia kufocus kwenye kazi zake zaidi