Mark Zuckerberg aahidi "kuirekebisha" namna ambavyo Facebook inashugulikia habari zisizo za kweli na matamshi ya chuki

Mkurungenzi mkuu wa Facebook, Mark Zuckerberg ameahidi "kurekebisha" Facebook ikiwa kama malengo yake binafsi ya mwaka 2018.
Katika ujumbe aliyoutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kuwa amefanya makosa mengi katika kutekeleza sheria na kuzuia utumiaji mbaya wa mtandao huo
Bw Zuckerberg ni maruufu kwa kujiwekea malengo binafsi kila mwaka tangu 2009. Facebook ilizinduliwa mwaka 2004.
Mitandao ya kijamii yamekoselewa sana kwa kuruhusu habari zisizo za kweli kusambazwa muda kabla ya uchaguzi wa Marekani.
Mtandao wa kijamii wa Facebook imekoselewa kwa kuruhusu matangazo yenye uhusiano na nchi ya Russia wakati wa kinyang'anyiro cha ugombea rais Marekani.
Bw Zuckerburg amesema atatia jitihada katika "maswala muhimu" aliyoyataja kama "kuilinda jamii yetu dhidi ya unyanyasaji na chuki, dhidi ya mataifa yanayoingia kati ya maswala ya mataifa mengine, na kuhakikisha kwamba muda unaotumiwa kwenye Facebook unatumiwa vizuri."
"Hatutaweza kuzuia makosa yote au unyanyasaji wote, lakini kwa sasa tumefanya makosa mengi katika kutekeleza kanuni zetu na kuzuia utamiaji mbaya ya vifaa vyetu" aliandika.
"Kama tutafanikiwa mwaka huu, basi tutaimaliza mwaka 2018 kwa muelekeo mzuri"

Baadhi ya malengo yake ya miaka iliyopita yalikuwa kuvaa tai kila siku na kuwinda na kuchinja chakula chake mwenyewe.
Lakini wakosoaji wametoa hoja ya maana ya yeye kuwa na malengo hayo.
Mmoja wapo, mwandishi wa maswala ya kiteknolojia Maya Kossoff, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, "Malengo binafsi ya Zuckerberg ya mwaka 2018 ni.. kufanya kazi ambayo anapaswa kuwa anafanya kama mkurungenzi mkuu wa Facebook. "

Malengo ya Mark Zuckerberg
2009 - Kuvaa tai kila siku
2010 - Kujifunza lugha ya kichina ya Mandarin
2011 - Kukula nyama ambayo amechinja mwenyewe
2013 - Kukutana na mtu mmoja kila siku nje ya Facebook
2015 - Kusoma kitabu kila wiki
2016 - Kutengeneza roboti wa kuendesha shughuli za nyumbani kwake

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post