Mapenzi Yamuhamisha Dini Kadja Nito Azidi Kumtibua Mama Yake

MREMBO wa Bongo Fleva, Natasha Lisimo ‘Kadja Nito’ ambaye aliingia kwenye bifu zito na mama yake baada ya kubadili dini na kuwa Mkristo na kumsamehe kipindi alipokuwa mahututi akijifungua, amemtibua tena mzazi wake huyo kutokana na kukomaa kwenye dini hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kitendo cha mama yake Kadja kumsamehe alipokuwa mahututi leba, aliamini baada ya kurejea kwenye hali yake ya kawaida huenda angemtii na kurudi kwenye Uislamu lakini ndiyo kwanza, dini ya Kikristo imemkolea na sasa anajianika waziwazi hadi mitandaoni, jambo linalomchefua mzazi wake huyo.

Kutokana na ishu hiyo Kadja alipoulizwa alisema; “Kuna vitu sipendi kuviongelea sana kwa sasa, hususan mambo yangu na mama yangu ni masuala ya kifamilia, kama mnaona najianika kwenye Ukristo na nilibadili dini nikawa huko, sioni kama kuna haja ya kuzungumzia hilo kwa kina

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post