DIVA: Atakaetaka kunioa Mahari Milioni 500




Breaking News Kiswahili

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za roho cha clouds FM Diva The Bwashe (pichani) amesema mwanaume yoyote anayetaka kumuoa aje na mahari ya shilingi za kitanzania milioni 500 na awe na upendo wa dhati.

Mtangazaji huyo maarufu, Mwanzo wengi walimfahamu kwa jina la Loveness Love, Lakini kwa sasa anatambulika sana kwa jina la Diva the bawse.

Mtangazaji huyo Maarufu wa kipindi cha Ala za Roho kupitia Redio Clounds Fm jana ametangaza mahali ya shilingi milioni mia tano kwa mwanaume anaetaka kumuoa baada ya kuachwa na aliyekuwa mpenzi wake.

Zaidi binti huyo wa Jamal Malinzi, Diva the bawse amesema ataangalia mwanaume mwenye Mapenzi ya kweli na mwenye roho nzuri kwa mwanamke.

Wajuzi wa mambo wanasema hizo ni hasira baada ya kutoswa live redioni ofisini kwake na aliyekuwa mpenzi wake aitwaye Heri Muziki.

Hasira hizo zimepelekea Diva kufungia wimbo wao mpya ambao walishirikiana kuuandaa usizinduliwe na kutambulishwa.

Diva ametoa dau hilo la million 500 kufuatia kujinadi kwake kuwa ndiye mzuri wa umbo na sura.

Nini maoni yako

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post